Klabu ya Manchester City imetuma ofa ya paundi milioni 40 kwenda kwa
klabu ya Liverpool kwa ajili ya kumnunua kiungo mshambuliaji raia wa
England Raheem Sterling .
Ofa hii inakuwa ya pili toka kwa City ambao wanaonekana kuwa
wamepania katika azma yao ya kumsajili kiungo huyu ambaye ametokea kuwa
moja kati ya wachezaji muhimu kwenye kikosi cha Liverpool na timu ya
taifa ya England katika siku za hivi karibuni .
Taarifa hii inakuwa sehemu nyingine katika mfululizo wa ‘filamu’
inayoendelea kati ya Raheem Sterling na Liverpool baada ya kiungo huyo
kuweka wazi kuwa amegoma kusaini mkataba mpya ndani ya timu hiyo
inayomilikiwa na wamarekani Fenway Sports Group .
Awali kuelekea mwishoni mwa msimu uliopita Sterling alifanya
mazungumzo yaliyorekodiwa na kituo cha BBC ambapo alifichua kuwa amegoma
kusaini mkataba mpya baada ya kutoridhishwa nao huku akionekana wazi
kuwa amejiandaa kuondoka.
Liverpool
imesema kuwa haitasikiliza ofa yoyote iliyoko chini ya oaundi milioni
50 ambayo wanaona ndio thamani halisi ya Raheem Sterling.
Wakala wa mchezaji huyo naye hakusita kuweka wazi kuwa mteja wake
atajiunga na moja kati ya wapinzani wakubwa wa Liverpool ambapo awali
ilivumishwa kuwa Manchester United na Manchester City zingeingia vitani
kusaka saini yake .
Manchester City hawakuchelewa ambapo haraka waliingia sokoni na
kupeleka ofa ya paundi milioni 30 ambayo Liverpool iliikatakaa kabla ya
kuja na ofa ya pili ambayo kama ya kwanza pia imekataliwa .
Liverpool wameweka wazi kuwa hawatasikiliza ofa yoyote ambayo iko
chini ya paundi milioni 50 ambazo wao kama klabu wameweka kama thamani
ya mchezaji huyo .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni