Mshambuliaji mpya wa klabu ya Manchester United Memphis Depay, anaweza
kujiingiza kwenye malumbano na muimbaji Chris Brown baada ya jana usiku
kupost picha akiwa katika pozi tata na ex girlfriend wa muimbaji huyo,
Karrueche Tran.
Depay ambaye amesajiliwa na United mapema mwezi uliopita, kwa sasa
yupo mapumzikoni nchini Marekani ambapo ndio amekutana na Karruache.
Ikumbukwe wiki kadhaa zilizopita mwanamitindo mkongwe Tyson Beckford
aliingia kwenye malumbano na muimbaji Chris Brown baada ya mwanamitindo
huyo kupost picha ya ‘selfie’ akiwa na mwanadada Karrueche Tran.
Chris Brown amekuwa na kasumba ya kugombana na kila mwanaume ambaye
anakuwa na ukaribu na Karrueche, alianza na Drake na kisha Tyson
Beckford.
Depay ambaye anatarajiwa kujiunga rasmi na timu yake mpya mapema mwezi
ujao, alipost picha hiyo na Karruache na hakuandika caption yoyote huku
akiwaacha mashabiki wake wakimsifia kwamba anapendezana na Msichana huyo
huku wengine wakimuonya juu ya Chris Brown.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni