Juma Ally akionyesha jeraha alilolipata baada ya kumwagiwa maji ya moto na mpenzi wake.
MAPENZI kiboko!
Juma Ally, mkazi wa Mongolandege Ilala jijini Dar es Salaam, amejikuta
katika wakati mgumu baada ya kumwagiwa maji ya moto na mpenzi wake,
Swaumu Shemsanga, kisa kikidaiwa kupishana kauli kwenye mazungumzo yao.
Chanzo makini kimelieleza gazeti hili
kuwa tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya Juma
kwenda kwa rafiki yake huyo na katika mazungumzo hayo, kudaiwa kuwa
mwanaume alimwambia mpenziwe kuwa huo ndiyo umekuwa mwisho wa mapenzi
yao.
Inadaiwa kuwa baada ya kauli hiyo,
mwanamke huyo alimmwagia maji ya moto mpenzi wake, ambayo wakati wa
mabishano alikuwa akiyachemsha.
Baada ya kumwagiwa maji hayo, majirani
waliwahi kumsaidia kwa kumpeleka polisi ambako alipewa hati ya matibabu
(PF 3) na kupelekwa katika Hospitali ya Amana iliyopo Ilala jijini Dar
es Salaam ambako alilazwa.
Polisi walifungua jalada lenye namba GMT/RB/1682/2015 KUJERUHI, ingawa taarifa kutoka hospitalini hapo hazioneshi aliungua kiasi gani.
Polisi walifungua jalada lenye namba GMT/RB/1682/2015 KUJERUHI, ingawa taarifa kutoka hospitalini hapo hazioneshi aliungua kiasi gani.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka
hospitalini hapo, Juma alisema yeye ana mke na watoto, lakini Swaumu
alikuwa ni mpenzi wake wa nje na wakati akienda nyumbani kwake, mkewe
alikuwa safarini Morogoro.
Aliongeza kuwa, Juni 10, mwaka huu
alikwenda kwa Swaumu kama alivyozoea lakini baada ya kufika katika
mazungumzo yao anadai kuwa walipishana lugha hali bila kujua kama
Swaumu angemfanyia kitendo cha kikatili namna ile.
Taarifa za kipolisi zinasema, Swaumu alikamatwa saa chache baada ya tukio hilo na uchunguzi wa suala hilo unaendelea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni