Toka mwaka uanze mastaa wengi wemeonekana kuingia kwenye headlines kuhusu mipango ya namna wanavyojiandaa kubaki juu 2015 kwa kufanya kazi nzuri, jitihada ambazo tunaziona pia kwa mastaa muziki pia.
Mkali kutoka Nigeria, Martins Okechukwu Joshua maarufu kama J Martins yeye kaonyesha ambavyo ameamua kuja na ujio mwingine mwaka huu, kwa wanaojua muziki wa Afrika Magharibi jina la Youssou N’dour sio geni, huyu ni mwanamuziki mkongwe toka Senegal, jarida la Forbes lilimtaja kwamba ndiye mwanamuziki tajiri zaidi Afrika 2014, pia ni Balozi na Waziri wa Utamaduni Senegal.
Mimi nausubiria mchanganyiko huu kwa hamu, story ni kwamba tayari kazi hiyo imeshafanytika na kwa sasa wako kwenye maandalizi ya kufanya video, wimbo unaitwa ‘Time Is Now’ , producer ni yeye mwenyewe J Martins.
Na hizi ni picha zilizopigwa wakati Video hiyo ikifanyika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni