Stori:Imelda Mtema na Musa Mateja
MAMBO si mambo! Tayari mimba ya muigizaji Aunt Ezekiel imeanza kumtibua baada ya nyota huyo kushindwa kufanya baadhi ya kazi ambazo alikuwa akizifanya mwenyewe.
Mose Iyobo akimsaidia kuvaa kiatu muigizaji maarufu Bongo, Aunt Ezekiel.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, kutokana na tumbo kuwa kubwa, Aunt kwa sasa hawezi kufunga viatu vyake, kufua, kuosha vyombo na hata akitaka kwenda toileti inabidi apewe kampani na mtu.
“Mh! Jamani Aunt hata kuinama ni mtihani sasa sijui kama ni kujidekeza au nini maana anapokuwa karibu na bebi wake ndiyo usiseme ni full kudeka anasema akiinama anaumia jamani?“Eti sasa hivi shosti wake Wema Sepetu na bebi wake Mose Iyobo ndiyo wamekuwa wakifanya kazi ya ziada kumsaidia kila kazi nyingi anazoshindwa,” kilisema chanzo hicho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni