GENN MEDIA

KANSAS COLLEGE OF NURSING

Ijumaa, 9 Januari 2015

Steven Gerard na Frank Lampard kama Tu Pac na Biggie.

big-and-2pac

Moja kati ya hoja ambazo zimekuwa zikijadiliwa sana na mashabiki wa soka nchini England hasa wale wa timu ya taifa ya England na klabu za Chelsea na Liverpool ni kuhusu ubora wa viungo wawili Steven Gerard na Frank Lampard .
Viungo hawa walikuwa viungo bora raia wa England katika kizazi chao na mashabiki walikuwa na matumaini makubwa ya kuwaona wakifanya vizuri wakiwa na timu ya taifa jambo ambalo halikuwahi kutokea .

Watu wengi wamekuwa wakihoji hivi , je ni nani bora kati yao  na wengi zaidi wamekuwa akibishana kuwa kwanini viungo hawa hawakuwahi kucheza katika ubora kwa pamoja wakiwa na timu ya taifa ya England na mpaka wanatangaza kustaafu kuichezea England jibu la swali hilo halijawahi kupatikana .

Hivi karibuni ubishi huu umeingia katika kiwango kingine na sasa umehamia nchini Marekani ambako utaanzishwa upya safari hii ukiwahusisha mashabiki wa soka nchini humo ambako mchezo wa soka bado sio mkubwa kulinganisha na michezo mingine kama American Football na mpira wa kikapu pamoja na Baseball.

Hii ni baada ya wachezaji hawa katika nyakati tofauti kusajiliwa na timu za marekani ambazo zinatarajiwa kuwa na upinzani wa jadi kuanzia msimu ujao wa ligi ya Marekani MLS .

Gerard na Lampard wamepata mafanikio makubwa wakiwa na klabu zao Liverpool na Chelsea.

Gerard na Lampard wamepata mafanikio makubwa wakiwa na klabu zao Liverpool na Chelsea.
Frank Lampard siku chache kabla ya kumalizika kwa msimu wa ligi ya England kwa miaka ya 2013/2014 alitangaza kujiunga na klabu mpya ya New York City Fc yenye makao makuu yake ndani ya jiji la New York .

Miezi kadhaa baadae Steven Gerard naye alitangaza kuwa angeachana na Liverpool baada ya kuitumikia kwa miaka 26 tangu akiwa na umri wa miaka 9 na taarifa hiyo ilifuatiwa na uthibitisho kuwa angejiunga na timu ya zamani ya David Beckham ya Los Angeles Galaxy baada ya kusaini mkataba wa miezi 18.

Nchini Marekani kumekuwa na upinzani mkubwa kati ya majimbo ya New York na Los Angeles , huu ni upinzani wa kitamaduni ambao umekuwa kwenye tasnia mbalimbali kuanzia tasnia ya burudani kwa maana ya muziki na filamu mpaka sasa kwenye michezo .

Wachezaji hawa wawili wameshindwa kufanya vizuri wakiwa pamoja kwenye timu ya taifa ya England .

Wachezaji hawa wawili wameshindwa kufanya vizuri wakiwa pamoja kwenye timu ya taifa ya England .
New York hupenda kujisifu kuwa mji mkubwa kuliko yote nchini marekani na alama halisi ya nchi hiyo na sifa hiyo hiyo pia imedaiwa kwa watu wa Los Angeles ambao hupenda kuwaaminisha watu kuwa jimbo la California ndio kitovu cha uzuri wa Marekani.

Gerard na Lampard wanaingia kwenye utamaduni wa upinzani huu ambapo wamefananishwa na wanamuziki nguli wa miondoko ya Hip-Hop ambao wote ni marehemu Christopher Wallace aka Notorious B.I.G na Tu Pac Amaru Shakur ambao walikuwa wapinzani wa jadi wakiwakilisha kambi za New York (Eastcoast) na Los Angeles California (West Coast).

Lampard na Gerard wamehamia klabu za Marekani na msimu uliopita watacheza kwenye ligi ya MLS.
Lampard na Gerard wamehamia klabu za Marekani na msimu uliopita watacheza kwenye ligi ya MLS.
Moja ya mambo ambayo yanangojwa ni jinsi ambavyo wachezaji hawa watakavyozibeba timu zao katika msimu ujao wa soka Marekani na moja ya sababu ambazo zimefanya wasajiliwe na timu hizi pamoja na ubora wao ni kuongeza umaarufu wa ligi ya soka ya marekani na mchezo wa soka kwa ujumla na gumzo ambalo wamelileta kimataifa hakika limeongeza umaarufu wa ligi hii.

Upinzani wa viungo hawa wawili unatarajiwa kuongeza umaarufu wa ligi ya soka Marekani na mchezo mzima kwa jumla.
Upinzani wa viungo hawa wawili unatarajiwa kuongeza umaarufu wa ligi ya soka Marekani na mchezo mzima kwa jumla.





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni