GENN MEDIA

KANSAS COLLEGE OF NURSING

Alhamisi, 15 Januari 2015

Rais wa Equatorial Guinea ameamua kutoa zawadi hii kwa mashabiki kuelekea AFCON

AFC

Michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika AFCON inatarajia kuanza rasmi January 17 Equatorial Guinea.
Rais wa nchi hiyo Teodoro Obiang Nguema ameamua kununua tiketi 40,000 ambazo zina gharama ya milioni 20 kwa ajili ya kuwapa mashabiki ambao hawatakua na uwezo wa kulipia tiketi ili kuweza kuona mashindano hayo.
“Lazima tuonyeshe kujali mashindano makubwa kama haya, tunahitaji kwenda kwa wingi uwanjani ili kujaza uwanja na kutoa hamasa “alisema mkuu huyo wa nchi.

RAI
Rais wa Equatorial Guinea Teodoro Obiang Nguema

Alisema ili kuongeza hamasa zaidi Serikali yake itatoa muda kwa wafanya kazi kutoka mapema ili kuweza kuhudhuria mechi zitakazokua zikichezwa siku za kazi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni