Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu cha ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu.

Kutoka uchinga hadi ubunge, Joshua Nassari mtoto wa mchungaji Nassari
KWA TAARIFA YAKO leo hii ni kuhusiana na faida ya kutoa fungu la kumi, lakini hapa tunachukulia mfano kutoka Mbunge Joshua Nassari, kutazama alipotoka na alipofikia. Katika mambo yote ambayo amekuwa akifanya, tokea alipoanza shule ya msingi Sinoni mwaka 1993, Mbunge Joshua Nassari amekuwa mwaminifu katika kutoa fungu la kumi. Na hilo KWA TAARIFA YAKO limemtoa kiroho na kimwili.
Yawezekana hufahamu, lakini KWA TAARIFA YAKO miaka ya 1995/1996 akiwa darasa la nne na la tano, kijana huyu alikuwa soko kuu Arusha akiuza machungwa, na mwaka 1996 pia alikuwa soko lo Kilombero na Ngaramtoni akiuza mifuko ya plastiki maarufu kama Malboro.
Pamoja na yote hayo, hata faida ndogo iliyokuwa ikipatikana katika biashara zake, hakuacha kutoa fungu la kumi, na hili ndilo lililopelekea kuinuliwa, maana amekuwa mwaminifu.
Kitabu cha Nahumu kinasema kuwa 'utafika wakati Mungu atakwenda kuinua waliodharauliwa'
Joshua Nassari, tokea umachinga mpaka mbunge - na KWA TAARIFA YAKO haya yote yasingetokea kama hakuwa mwaminifu kwenye fungu la kumi, na bado anaendelea kuwa hivyo.
Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO kama ulikuwa hujui,
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni