GENN MEDIA

KANSAS COLLEGE OF NURSING

Alhamisi, 15 Januari 2015

Kama ungependa kusikiliza story kutoka Kenya, hapa kuna story zote za Kenya kutoka Radio Jambo

free_desktop_wallpaper_logo_radio_news_1024x768

Hii ni habari kutoka Kenya, ilirekodiwa wakati ikisomwa hewani Radio Jambo, unaweza kufahamu story zote za Kenya leo January 15 baada ya kupitia hapa.
Baadhi ya taarifa zilizosikika kwenye Habari hiyo ni pamoja na Afisa wa Polisi na mtuhumiwa wa wizi wamefariki baada ya kupata ajali ya gari wakiwa wanaenda kukamata vitu vya wizi katika barabara inayotoka Nairobi kwenda Namanga, huku askari wengine watatu wakijeruhiwa kutokana na ajali hiyo iliyohusisha gari mbili ambazo zilikuwa zikiendeshwa na askari hao na gari moja kubwa ambazo ziligongana.
Abiria mmoja ameuwawa kwa kupigwa risasi na wengine watano kujeruhiwa vibaya baada ya basi lao kuvamiwa na kurushiwa risasi eneo la Lami Nyeusi.
Rais Uhuru Kenyatta leo ameongoza mkutano wa Baraza la Mawaziri katika Ikulu ya  Nairobi ukiwa ni mkutano wake wa kwanza kwa mwaka 2015.
Jeshi la Polisi Kenya bado liko katika msako wa magari yaliyo na ving’ora kinyume cha sheria ambapo gari za ambulance, Polisi na Vikosi vya Zimamoto pekee ndivyo vinaruhusiwa kuwa na ving’ora hivyo.
Bonyeza play kusikiliza Habari zote za leo Jan 15 kutoka Redio Jambo ziko hapa.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni