Huu ni ubunifu ambao hata mimi umenivutia, nakumbuka mwaka 2012 rapper Jay Z aliwahi pia kusurprise kwa kuingia kwenye treni ya abiria halafu akaendelea na safari, huku aliyekaa naye kiti kimoja alikuwa bibi mzee ambaye hata hakujua kwamba amekaa na staa mkubwa duniani!
Mariah Carey naye amekuja na hii kwa fans wake Las Vegas, mashabiki wake walikuwa wakihojiwa ndani ya vyumba vya hoteli, wakaeleza namna ambavyo wanamkubali staa huyo, halafu ghafla mlango unagongwa na mtu ambaye anajitambulisha kuwa ni mhudumu wa hoteli, halafu wanapogeuka kumuangalia mhudumu wanakuta mhudumu huyo ni Mariah Carey mwenyewe!
Hii imenivutia, katika surprise hiyo fans wake hao walipata nafasi ya shavu la ticket za show yake ambayo ataifanya May 6 Las Vegas, Marekani.
“Hili ni tukio muhimu kwangu na tena nina imani mashabiki wangu wataifurahia hii kwa sababu naenda kufanya shoo ambayo ni kama njia ya kuiongoza album yangu ambayo ni toleo la 18, naamini watu wengine watafurahia kwa sababu sijawahi kufanya hivi kabla“ — Mariah Carey.
Video na pichaz za surprise hiyo ziko hapa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni