Ni mara ngapi imetokea unapoteza kitu na kukipata baada ya mtu kukiokota?
Jamaa mmoja ambaye ni mtengeneza Filamu raia wa Uingereza amefanya utafiti katika mitaa ya Dubai, utafiti ulioitwa “Je unaweza kuiba Dubai?” kwa lengo kuangalia jinsi gani watu wa maeneo ya huko ni waaminifu.
Jamaa huyo Daniel Jarvis, akiwa na rafiki yake walianza utafiti huo hivi karibuni kwa kuficha camera na kurekodi mfululizo wa matukio, Daniel anapita mtaani halafu anaangusha wallet yake makusudi kabisa, ili kuangalia wale watakaoiona watachukua uamuzi gani?
Mtaa wa kwanza walioufanyia majaribio hilo ni katika barabara ya Sheikh Zayed karibu na Soko Kuu la kibiashara na jirani kabisa na mnara wa Emirates, kila aliyeiona wallet hiyo alimrudishia, akahisi huenda sababu ya kurudishiwa pochi hiyo ni kutokana na wakazi wa eneo hilo kuwa matajiri, wakaamua kuhamishia utafiti huo eneo la Bur, ambalo watu wa maeneo hao ni wale wenye kipato cha kawaida, cha kushangaza watu hao pia walimrudishia.
Kikubwa kilichomshangaza katika utafiti huo ni kwamba hata watu waliookota pochi hiyo hawakujishughulisha kutazama ndani kuna nini, walimuita na kumpatia!
Kampuni hiyo ya utafiti ya Trollstation inaendelea na utafiti wake katika Falme za Kiarabu, Ulaya, Marekani na hatimaye Afrika ambapo wamesema huenda maeneo watakayopita yakavunja rekodi ya Dubai.
Nasubiri kama utafiti huu ukifika Tz, maeneo ya watu wengi kama Kariakoo, unadhani hali itakuwaje mtu wangu?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni