Matukio ya kuuawa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi albino bado yameonekana kuendelea kuchukua nafasi hasa katika Mikoa ya kanda ya Ziwa hali inayozidi kutishia amani kwenye familia nyingi.
Waziri wa mambo ya Ndani Mathias Chikawe ametoa tamko kuwa kutakua na operesheni ya kitaifa ya kuwasaka na kuwakamata waganga wa kienyeji wanaojihusisha na kupiga ramli ili kuwafikisha mahakamani.
Uamuzi wa Waziri huyo unatokana na kukithiri kwa vitendo vya unyanyasaji wa watu wenye ulemavu vikishika kasi kutokana na kuuawa kwa imani za kishirikina.
Chikawe alisema watashirikiana na Chama cha watu wenye ulemavu kuwabaini wahalifu na kuwachukulia hatua ili kupunguza vitendo hivyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni