GENN MEDIA

KANSAS COLLEGE OF NURSING

Ijumaa, 19 Desemba 2014

Hali ya hewa ilichafuka ndani ya Bunge Kenya leo… Tazama Video na Pichaz hapa

Ke2

Kikao cha Bunge la Kenya kilisimama kwa takribani dakika 30 kutokana na kutofautiana kwa Wabunge hao kuhusiana na msimamo wao kutofautiana wakati wakiendelea na mjadala unaohusu mabadiliko ya Sheria ya Usalama wa Nchi hiyo kutokana na kukabiliwa na changamoto mbalimbali kwenye masuala ya Usalama.
Wabunge wa upinzani walipinga muswada huo kwa kutupa karatasi chini, Bunge likaahirishwa ambapo hali ya hewa ilikuwa mbaya na baadaye Wabunge hao kupigana, wengine wakichaniana nguo na hata kuumizana.

Ke

Vikosi vya Usalama vililazimika kulizunguka eneo hilo la Bunge ili kuimarisha Usalama.

Ke00

             Seneta Johnston Muthama alichaniwa nguo na kuumizwa katika vurugu hizo.

Ke1
                                    Hali ilivyokuwa nje ya Bunge la Kenya leo.

Wabunge wa Upinzani waligomea muswada huo na kuanza kuimba, Bunge hilo likasitishwa.
Nimekurekodia sauti wakati habari hiyo ikiripotiwa na kituo cha WBS unaweza kubonyeza play kuisikiliza, pia kuna video kutoka K24 ambayo unaweza kuitazama hapa.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni