GENN MEDIA

KANSAS COLLEGE OF NURSING

Ijumaa, 19 Desemba 2014

Habari njema kwa madereva, saa ya mkononi itaweza kuiongoza gari sehemu ya parking

usukan

Hakuna kitu kibaya kama kusahau ulikoegesha gari lako, hasa kwa maeneo ambayo kumekuwa na tatizo la wizi wa magari, moja kwa moja unaweza kuazna kuhisi kwamba gari yako imeibiwa…….. wameandika BBCswahili
Lakini sasa kero hiyo inaweza kubaki historia kwani kampuni ya kutengeza magari ya BMW, imetangaza kuzindua kifaa ambacho kinaweza kuyawezesha magari ya kampuni hiyo kujiegesha yenyewe kwa kubonyeza kifaa hicho.
Hata hivyo dereva atalazimika kuvaa saa ya Smartphone mkononi ambayo itamsaidia kuiongoza gari hiyo kwa sauti mpaka sehemu ya parking.

bmw

Gari hilo kwa amri ya dereva litatoka liliko baada ya dereva kushuka na kwenda lenyewe kwa kuhesabu muda utakalichukua kwenda kutafuta sehemu ya kujiegesha.
Tawi la kampuni ya BMW mjini Munich, Ujerumani limezindua teknolojia hiyo ambayo itawezesha gari kujiegesha lenyewe na itaanza kufanya kazi mwezi ujao.
saa



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni