GENN MEDIA

KANSAS COLLEGE OF NURSING

Jumamosi, 6 Septemba 2014

OKWI AWA KIVUTIO MAZOEZI SIMBA, AONYESHA MAKALI, MASHABIKI WAKUBALI


Kiungo mshambuliaji Emmanuel OKwi aliyeingia mkataba wa miezi sita na Simba, amekuwa kivutio kwenye mazoezi ya kikosi hicho.

Katika mazoezi ya Simba yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uninio, Bunju jijini Dar, Okwi alikuwa kivutio kutokana na kasi na chenga zake za maudhi.
Mashabiki wengi waliojitokeza walionyesha kuvutiwa naye na wakati mwingine walimpigia makofi kuonyesha kukubali alichokuwa akifanya.
Okwi anatarajia kuwa katika kikosi cha Simba kitakachoivaa Gor Mahia kwenye Uwanja wa taifa katika mechi ya kirafiki leo jijini Dar.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni