KITUKO! Msanii wa sinema za Kibongo, Coletha Raymond ‘Koleta’ ametoa kali ya aina yake kwa kusema anapenda ujauzito kiasi cha kufikia hatua ya kujaza matambara tumboni ili awe na muonekano wa mjamzito.
Akizungumza na paparazi wetu, Koleta alisema kwa jinsi anavyopenda ujauzito, akimuona mwanamke yeyote mjamzito anamfuata na kuzungumza naye hata kama hamfahamu na kama yuko jirani ataenda kukaa naye.
Mwanadada kutoka tasnia ya filamu Bongo, Coletha Raymond ‘Koleta’
“Sijui kwa nini na kuna wakati mwingine naweka matambara tumboni naweza kuzunguka nayo siku nzima kama mama mjamzito yaani huwa najicheka mwenyewe,” alisema Koleta huku akidai akitokea mwanaume watakayeendana basi atambebea ujauzito.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni