Kampuni ya Britts Event iliyohusika kuandaa show ya Diamond Stuttgart, Ujerumani imeeleza kwa kina kiini cha vurugu kubwa zilizotokea kwenye show hiyo na kusababisha uharibifu mkubwa huku baadhi ya watu wakijeruhiwa vibaya.
Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hiyo, Awin Williams Akpomiemie ameeleza kwa kina kuhusu mzozo uliokuwepo ndani ya kampuni hiyo ulioathiri show hiyo kwa ujumla.
Hiki ndicho alichokisema:
Watu wangu awali ya yote, ningependa kuelezea moyo wangu kwa kuuambia umma na mashabiki wa Diamond Platnumz, kwamba sisi kutoka uongozi wa Britts Events tunaomba radhi kwa kile kilichotokea usiku uliopita, wakati wa show ya Diamond Platnumz.
Haikuwa imepangwa show ichelewe kuanza au kwa msanii kutotumbuiza. Hapa ntawaeleza ukweli wote wa kile kilichotokea katika tamasha hilo kwakuwa ninyi nyote mnataka kuujua ukweli.
Mradi wa Diamond ulikuwa wa gharama kubwa sana kwakuwa uongozi Britts Events ulitaka kila kitu kiwe professional. Kama kampuni tuliamua kutafuta wawekezaji watakaowekeza kwenye mradi huu hivyo tuliwafuata wawekezaji watatu lakini mmoja wao hakuwekeza sana kwani alidai hatokuwa nchini.
Wawekezaji wawili ni watu wanaofahamika sana jijini Stuttgart, mmoja anafanya kazi na jeshi la Marekani na mwingine anamiliki kampuni ya usafirishaji mjini Stuttgart. Hawa ndio wawekezaji wakubwa tuliowapata.
Tuliwapa mikataba wasaini lakini yule mwenye kampuni ya usafirishaji alikataa kusaini mkataba wa mradi huo kwakuwa alitaka kuwa na mkataba wake binafsi na yule jamaa wa Marekani. Kisha nilimwambia Mr.USA kuwa hiyo haikuwa hatua sahihi lakini Mr.USA alisema ‘Britts msiwe na shaka, kila kitu kitakuwa poa.
Watu wangu, mradi ulianza na kisha wale wawekezaji wawili wakagundua kuwa Diamond ni msanii mkubwa na angevuta umati mkubwa wa watu na watu wanampenda.
Kisha walijiunga pamoja dhidi ya Britts waliowaalika kama wawekezaji kwenye mradi huo na walitaka kuuchukua kutoka kwa Britts sababu ni wao ndio walioleta sehemu ya fedha kwaajili ya mradi huu wakati Britts ndio wanaommiliki msanii na mradi wenyewe.
Ila tu kwakuwa Britts ni kampuni mpya mjini Stuttgart, Mr. Shipping Guy aliamua kuungana na yule jamaa wa Marekani na DJ Wanted, kuuchukua mradi.
Pindi Britts ilipokaa chini na kufanya mkutano nao, walikuwa wakifanya mkutano wao wenyewe na kubadilisha mipango yote hivyo walikuwa wanahujumu na kuendelea na mradi nyuma ya Britts.
Britts ina makubaliano nao kuwa pindi msanii atakapowasili Ujerumani, watampa balance ya 3.250 euros, na walikubaliana na kigezo hicho kwasababu Diamond aliweka wazi kuwa bila fedha asingepanda ndege.
Waliniomba mimi niongee na Diamond kuwa watampa fedha kwenye uwanja wa ndege, lakini unajua nini? Kabla Diamond hajawasili Mr. USA na Mr. Shipping Guy pamoja na DJ Wanted walitaka kuandaa wahuni kumuiba msanii kutoka kwenye show ya Britts lakini Britts walikuwa wajanja na walimchukua msanii kabla hawajafanya chochote. Hapo ndipo shida ilipoanzia.
Huko Essen kabla Britts haijafika huko, USA Guy na Shipping Guy, walikuwa wameshapeleka wafanyakazi wapya kuchukua show na kuwafukuza wafanyakazi wa mwanzo.
Kisha Britts ilikuwa ikilumbana nao kuwa wao ni wawekezaji tu na sio waratibu wa kampuni, kwanini wanataka kuhodhi tukio kwasababu mnataka kutengeneza fedha na sio kujali watu. Britts baadaye ilikuja kugundua kuwa wafanyakazi waliowapeleka walikuwa wapenzi wao wa zamani na ndugu zao.
Dhumuni la kufanya hivyo lilikuwa ni kuiba fedha na kutofuata mkataba na Britts, hivyo baada ya Diamond kuwasili Stuttgart usiku wa saa tano, alikuwa amechoka lakini wawekezaji hawakujali. Walikuwa wakifirikia tu jinsi wanavyoweza kurudisha fedha zao. Diamond alisema anahitaji fedha yake lakini Shipping Guy na USA Guy walikataa kumpa fedha Diamond wakihisi kuwa Britts wanataka fedha ya ziada.
Kisha usiku ulipoingia sana, waliweza kutoa 3.000 euros na ilikuwa saa tisa na nusu tayari lakini Diamond aliendelea kukataa kutumbuiza kwakuwa alidai ni lazima wamlipe fedha iliyosalia ambayo ni 250 euros, kitu ambacho ni haki yake kutokana na makubaliano.
Mpaka muda Mr Shipping Guy na Mr USA Guy wanagundua kuwa Britts walikuwa wakifanya kitu sahihi kwa kuwaomba walipe fedha hizo kwa Diamond, tulikuwa tumeshachelewa na watu walikuwa wameshaanza kupigana wakati huo Diamond alikuwa ndani ya gari mbele tu ya ukumbi, na kama ningemruhusu atoke wangemuua.
Tunavyoongea hapa, Mr USA anadai kuwa fedha tulizoingiza kwenye tukio zima ziliibwa na watu hivyo Britts Events haiwezi kupata fedha kutoka kwenye tukio tuliloliandaa na kulimiliki. Hiyo ilikuwa mipango yao kuchukua biashara ya mtu mwingine kutokana na tamaa.
Britts Events inawapenda, Britts Events ilitaka kila mtu awe na furaha, Britts Event haijawahi kuahidi msanii yeyote na asije. Na niamini hata tulipofanya show ya Bracket tulikuwa na kitu kile kile kutoka kwa wawekezaji. Walipoona kuwa show inaweza kuwa na mafanikio walitaka kupewa asilimia 50% ya kampuni.
Well, sitakiwi kusema yote haya kwakuwa ni jambo la uongozi lakini niliamua kuweka mambo sawa, siwezi kuficha tena. Tuna Waafrika wengi wenye tamaa wanaotaka kuchukua biashara za watu wengine sababu ya tamaa.
Lengo letu ni kuwafanya muwe na furaha na sio kupoteza muda na fedha zenu. Tunafahamu kuwa nyote mlitoka sehemu za mbali, mliacha watoto wenu na familia.
Uongozi wa Britts Events unaomba radhi kwa hili. Hivyo msiilamu Britts Events lakini laumuni tamaa za Mr. USA Guy na Mr. Shipping Guy. Tunawapenda na tunaahidi show ya bure ya Diamond hivi karibuni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni