Diamond Platinumz na uongozi wake wameridhia ombi la promoter wa Stuttgart, Ujerumani na msanii huyo atafanya show ya bure September 20 kwa lengo la kuwafidia mashabiki waliofanya vurugu baada ya kutoridhishwa na utaratibu wa show yake mwezi uliopita.
Mwimbaji huyo wa MdogoMdogo ameweka wazi uamuzi wa kurudi Ujerumani kupitia Instagram.
“YES!!!! STUTTGART GERMANY!!! on this 20th of September 2014... kiukweli nilisikitishwa sana na kilichotokea last time Stuttgart... lakini baada ya kugundua kuwa pia lilikuwa ni kosa la mtu mwingine na si promotter kama nilivyodhani, yaani Brittis Events... ndipo tulipoamua na kuwaletea Burudani hii Mashabiki zetu pendwa wa Stuttgart....hakikisha ufikapo unapendeza zaidi maana kama ujuavyo safari hii Vyombo vyote vya habari ndani na nje ya nchi vitakuwa pale kwa RedCarpet.... kiingilio ni BUREEEEEE!!!... tafadhariwambie na wenzio wa nchi za karibu...#NORWAY #HOLLAND #SWITZLAND #BELGIUM #SWEEDEN na kadharika!!!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni