GENN MEDIA

KANSAS COLLEGE OF NURSING

Alhamisi, 7 Agosti 2014

VIDEO: AKON ADAI NDOA YA JAY Z NA BEYONCE NI BIASHARA, THE CARTERS WAKAA KWENYE HOTELI YA TSH.50 KWA SIKU 1.

Wakati ambapo tetesi za kukaribia kuvunjika kwa ndoa ya Jay Z na Beyonce zikiendelea kushika kasi, msanii mwenzao, Akon amezungumza anachokiona kuhusiana na uhusiano wa mastaa hao. 

“Uhusiano wao umekuwa wa kibiashara katika ulimwengu wa nje kuliko uhusiano wa kawaida,” Akon alimwambia mwandishi wa TMZ aliyemuuliza anauonaje uhusiano wa Jay na Bey. “Ukiwa mtu unayejulikana na una uhusiano, uhusiano wako nao unakuwa wa umma. Hivyo usipofunguka kwa umma, ni kawaida wao kuongea vitu wanavyohisi vinaendelea,” aliongeza. Katika hatua nyingine, licha ya fununu za talaka mbele yao, Jumanne hii Beyonce na Jay Z walipiga show ya kufa mtu San Francisco, Calif. 


Wanandoa hao walidaiwa kukaa pamoja kwenye hoteli ya kifahari ambayo kwa chumba kimoja (presidential suit) gharama ni $30,000 (zaidi ya shilingi milioni 50) kwa usiku mmoja. Beyonce na Jay Z walikuwa pamoja jioni ya juzi kwenye hoteli ya kifahari St Regis hotel jijini San Francisco, kwa mujibu wa Daily Mail. 

Moja ya sehemu kwenye hoteli hiyo Wawili hao walikuwa na mtoto Blue Ivy Carter.