GENN MEDIA

KANSAS COLLEGE OF NURSING

Jumapili, 17 Agosti 2014

TANZANIA HAINA UGONJWA WA EBOLA, UDHIBITI VIWANJA VYA NDEGE NA MIPAKANI WAIIMARISHWA.

Mtaalam wa ufuatiliaji wa magonjwa ya binadamu wa wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Vida Mmbaga akitoa ufafanuzi kuhusu historia ya ugonjwa wa Ebola, Virusi vyake , dalili na namna unavyoenea wakati wa mafunzo maalum kwa waandishi wa habari kuhusu ugonjwa huo jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi wa Ufuatiliaji wa Magonjwa ya Binadamu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Janeth Mghamba akifungua  wa mafunzo maalum kwa waandishi wa habari kuhusu ugonjwa ugonjwa wa Ebola jijini Dar es salaam.

Afisa Afya Mkuu kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anayeshughulikia maeneo ya Bandari, Viwanja vya ndege na mipakani Dkt. Chacha Mung’aho  akizungumza namna walivyojipanga kukabiliana na tishio la ugonjwa wa Ebola  kupitia wasafiri wanaoingia nchini Tanzania.

Sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo hayo.





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni