GENN MEDIA

KANSAS COLLEGE OF NURSING

Jumapili, 17 Agosti 2014

LIVERPOOL 2 SOUTHAMPTONS 1

Sturridge akifunga goli la ushindi

LIVERPOOL imeanza vizuri Ligi Kuu ya England baada ya kuifunga mabao 2-1 Southamptons Uwanja wa Anfield jioni hii, ikicheza mechi ya kwanza ya ligi bila Luis Suarez iliyemuuza Barcelona. 
Shukrani kwake, mshambuliaji wa kimataifa wa England, Daniel Sturridge aliyefunga bao la ushindi  dakika ya 79 na kumpa mwanzo mzuri Brenden Rodgers aliyeukosakosa kidogo ubingwa msimu uliopita akizidiwa kete na Manchester City.
Sterling akifurahia goli alilofunga

Mechi hiyo dhidi ya Southampton haikuwa lelemama na Raheem Sterling na Dani Sturridge ndiyo walikuwa mashujaa kwa kufunga mabao mawili.
Bao pekee la Southampton la mkwaju mkali kama 'moto' lilifungwa na Clyne.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni