GENN MEDIA

KANSAS COLLEGE OF NURSING

Jumatano, 6 Agosti 2014

Kingine kilichomtokea Masogange ndani ya uwanja wa ndege Dar es salaam.


Video model Agnes Masogange mwaka jana alitawala vyombo vya habari baada ya kukamatwa na polisi huko South Africa akiwa na mwenzake Melisa Edward wakiwa na mzigo uliotajwa kuwa dawa za kulevya wenye thamani ya Tsh bilioni 6.8.
Taarifa mpya kutoka kwa kamanda wa polisi kitengo cha kuzuia na kupambana na dawa za kulevya Gedfrey Nzowa inasema kikosi hicho kilimshikilia Masogange usiku wa juzi baada ya kurejea akitokea South Africa.
Taarifa inasema kwamba Masogange alihojiwa kwa zaidi ya masaa 10 na kupekuliwa na baadae kuachiwa hutu bila masharti ambapo Masogange alivyotafutwa kwenye simu alijibu kwa kifupi na kusema,”hilo unalosema siyo kweli na sipo tayari kuzungumzia, siwezi kuzungumza na chombo cha habari kwa sasa shida yako nini”.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni