GENN MEDIA

KANSAS COLLEGE OF NURSING

Jumatano, 20 Agosti 2014

Kenya na Iran kuimarisha zaidi uhusiano

Amina Mohammad (kushoto) na Mohammad Javad Zarif

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Kenya zimetangaza kuwa tayari kuimarisha  zaidi uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi mbili.
Mawaziri hao wamejadili masuala ya uhusiano baina ya nchi mbili na pia masula ya kieneo na kimataifa. Mawaziri hao pia wamebadilishana mawazo kuhusu ushirikiano katika kukabiliana na wimbi la misimamo mikali duniani.

Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuna udharura wa kuimarishwa uhusiano wa Iran na nchi za Kiafrika. Zarifa ameyasema hayo leo hapa Tehran alipokutana na mabalozi wa Iran katika nchi za Kiafrika. Waziri wa mambo ya nje wa Iran amesema kuna fursa mbali mbali za kuimarisha uhusiano wa Iran na Afrika. 

Amesema kuimarisha uhusiano na nchi za Afrika ni katika misingi ya sera za kigeni za Iran na ametaka  sekta binafsi ya Iran ieneze shughuli zake Afrika. Ameongeza kuwa Iran iko tayari kuzipa nchi za Afrika uzeofu wake katika sekta za kiufundi, uhandisi n.k. Zarif amesisitza kuwa kinyume na baadhi ya nchi za kigeni,  uhusiano wa Iran na Afrika umejengeka katika msingi wa maslahi ya pande mbili.

-IRIB

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni