GENN MEDIA

KANSAS COLLEGE OF NURSING

Ijumaa, 22 Agosti 2014

Daesh Mwingereza ndiye aliyemchinja Mmarekani

Kufuatia kuenea picha za kukatwa kichwa mwandishi wa habari wa Kimarekani na mwanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh huko nchini Iraq, walimwengu wamewataja wanachama wa kundi hilo kutoka Uingereza kuwa ndio makatili zaidi. Hayo yamethibitishwa katika ripoti ya kituo cha kimataifa cha utafiti wa misimamo mikali cha King London na kuongeza kuwa, raia wengi wa kigeni wanaoelekea Syria wanakwenda kwa ajili ya kushiriki kikamilifu katika vita.

 Shahir Mahir, mtafiti katika kituo hicho amesema kuwa, yeye na wenzake wanaendelea kufuatilia uraia wa gaidi aliyemkata kichwa James Foley, mwandishi wa habari wa Kimarekani anayedhaniwa kuwa ni Mwingereza. Hayo yamekuja baada ya duru mbalimbali duniani kumtaja muhusika wa mauaji ya Foley kuwa ni raia halisi wa Uingereza. Habari zinaeleza kuwa, baada ya kuenea picha za gaidi huyo Waziri Mkuu wa Uingereza, David William Cameron, alivunja safari yake na kuerejea kwenye ofisi yake ya Downing Street.

Msemaji wa Waziri Mkuu huyo amesema kuwa, kufuatia hali hiyo kiongozi huyo anatazamiwa kujadili kwa kina na Waziri wa Mambo ya Nje, viongozi wa ngazi za juu serikalini na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi hiyo kuhusiana na hali ya mambo nchini Iraq na Syria, na kadhalika tishio la magaidi wa Daesh. 

Hii ni katika hali ambayo Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Philip Hammond, amekiri kuwa inavyoonekana, mtu aliyetekeleza jinai ya kutisha ya kumkata kichwa mwandishi wa habari wa Marekani, ni raia wa Uingereza. Aidha amesema kuwa, kuna uwezekano mkubwa kwamba raia wengi wa nchi hiyo, walishiriki katika jinai hiyo. 

Hivi karibuni Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, alinukuliwa na gazeti la Sunday Times akisisitiza kuwa, ikiwa mizizi ya kundi hilo la Daesh ambalo ni hatari, haitokatwa mapema zaidi, basi wanachama wa kundi hilo watawalenga 

Waingereza katika mitaa ya nchi hiyo. Kwa mujibu wa habari, ndani ya kipindi cha miaka miwili iliyopita, Waingereza 400 walisafiri nchini Syria kwa lengo la kushirikiana bega kwa bega na makundi mengine ya kigaidi yanayopigana kwa lengo la kuiangusha madarakani serikali halali ya Rais Bashar al-Assad wa nchi hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni