GENN MEDIA

KANSAS COLLEGE OF NURSING

Jumatano, 4 Juni 2014

Ukosefu wa damu salama wachangia asilimia 50 ya vifo vya wajawazito



 VIFO vya wanawake wajawazito vilivyotokea wakati wa kujifungua katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, katika kipindi cha mwezi Aprili, 2014, imebainika kuwa asilimia hamsini (50) ya vifo hivyo vilisababishwa na ukosefu wa damu salama katika Hospitali hiyo.

Daktari bingwa wa Magonjwa ya Wanawake, Dk. Geles Kamugisha, amesema hayo, Mei 28, 2014 kuwa, wananchi wanatakiwa kuwa na upendo wa kutambua umuhimu wa kutoa damu kwa ajili ya kusaidia akina mama kuondokana na tatizo hilo.

Amesema serikali inatakiwa kupitia upya sheria inayowabana baadhi ya watu wanaouza damu na kudhibiti hali hiyo, kwani huduma zitolewazo bure katika sekta hiyo zinawanufaisha watu wachache kinyume na utaratibu na waweze kuchukuliwa hatua kali huku akisema kufanya hivyo kunawakatisha tamaa wachangiaji wa damu salama.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa mpango wa damu salama katika hospitali hiyo, Dk. Abdul Juma, ameiambia FikraPevu kuwa ili tatizo hilo liweze kutatuliwa mpango huo unategemewa kuwashirikisha baadhi ya viongozi wa dini ili kuwaeleza ukubwa wa uhaba wa damu salama pamoja na athari zake, ili waweze kuwahamasisha waumini wao wajitolea damu na kunusuru maisha ya watu wanaokosa huduma hiyo. Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imesema kuwa zaidi ya asilimia 40 ya watoto wachanga nchini, wamekumbwa na ugonjwa utamiamlo na udumavu kwasababu ya kukosa huduma lishe bora katika kipindi kinachotakiwa hali inayoigharimu serikali kuanza kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kutoa huduma hiyo kwa watoto.



Mkurugenzi wa mafunzo kutoka katika Wizara hiyo, Hutlisia Kauze, amesema kutokana na ongezeko la tatizo hilo nchini, serikali imeanza kutoa elimu katika mikoa yote nchini ili kutoa elimu juu ya huduma bora wanazotakiwa kupewa watoto na kuweza kupunguza tatizo hilo kwa asilimia hamsini katika kipindi kifupi.

“Elimu zaidi inatakiwa kutolewa kwa jamii ili kunusuru watoto kukumbwa na tatizo hilo ambalo limeonekana kukumba nchi nyingi hususani zile zinazoendelea” alisema Kauze.

Tanzania bado ina kiwango cha juu cha wanawake wanokufa wakati wakijifungua, ambapo wanawake 454 kati ya laki moja hupoteza maisha kila mwaka, huku juhudi za serikali kwa kushirikiana na Wizara ya Afya ikifanya jitihada mbalimbali za kutaka kupunguza idadi hiyo hadi kufikia vifo 68 katika elfu moja.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni