Uwanja wa vita’ ulikuwa ni kwenye msiba wa mwigizaji mwenzao Sheila Haule ‘Recho’, Sinza-Palestina, jijini Dar ambapo chanzo kilishuhudia mtiti huo, kilidai tatizo liliibuka mara baada ya Steve Nyerere kumchimba mkwara Baba Haji asijiweke karibu na Jacob Steven ‘JB’.
Muigizaji mkongwe wa Bongo Muvi, Adam Haji ‘Baba Haji’ (kushoto) akishiriki kubeba jeneza lenye mwili wa marehemu Recho.
“Hata haikujulikana kwa nini Steve hakutaka Baba Haji awe karibu na JB, akammaindi ndipo mtiti ulipoibuka, wakataka kushikana mashati bahati nzuri Mtitu (William) akawaamua,” kilieleza chanzo.
Akizungumzia sakata hilo baada ya kutulizwa ‘munkari’, Baba Haji alisema anamshangaa Steve kwa kumchimba mkwara asikae na JB pasipo kuwa na sababu za msingi.
Sijui jamaa vipi, au ananionea wivu, nashindwa kumuelewa,” alisema Baba Haji huku Steve akichomoa kuzungumza lolote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni