GENN MEDIA

KANSAS COLLEGE OF NURSING

Jumatatu, 4 Agosti 2014

RAIS KIKWETE NA MARAIS 46 WA AFRIKA WAKUTANA NA RAIS OBAMA


Rais Jakaya Mrisho Kikwete  yuko  Marekani kwa ziara ya siku tisa nchini humo ambako ni miongo mwa  mambo mengi, atahudhuria mkutano wa kwanza wa kihistoria wa viongnzi wa Bara la Afrika na Marekani ulihitishwa na Rais Barack Obama.

Mkutano huo wa siku mbili unafanyaika kuanzia leo ukianza na mkutano wa biashara kati ya Afrika na Marekani.

Utakaofatiwa ni mkuta wa wenyewe Marekani na Afrika utakaofanyika Wizara ya mambo ya Nje
ya Marekani.
Kwenye uwanja wa Ndege wa kimataifa Dulles mjini Washington, Rais Kikwete alipokelewa na Balozi wa Tanzania Marekani, Liberata Mulamula na maofisa kutoka Wizara Mambo ya Nje ya Marekani.
Kwenye ziara hiyo, Rais Kikwete ameongozana na Mkewe,Mama Salma Kikwete ambaye na ye atakuwa na program tofauti wakati wa ziara hiyo kama watakavyokuwa wake wa viongozi wengine wa Afrika wanaohudhuria mkutano huo.

Mkutano huo wa kwanza ni wa aina yake kiongozi wa Marekani na Viongozi wa Afrika umepangwa kuhudhuriwa na Viongozi 47 kutoka Afrika ambazo zote zimealikwa na Rais  Obama kushiriki mkutano huo.
Mbali na shughuli zake za mjini Washington, Rais Kikwete atasafiri kwenda Dallas, Jimbo la Texas ambako atakutana na Rais wa 43 wa Marekani, George W. Bush, kabla ya kuendelea na safari katika mji mwingine mkubwa wa jimbo hilo Houston.

Mjini Housto, Rais Kikwete atafanya mkutano wa kimkakati wa kibiashra na wafanyabishara maarufu mabali mbali hasa wa sekta ya gesi na mafuta kabla ya kumaliza ziara yake.

Miongini mwa shughuli zake, Mama Salma Kikwete atahudhuria mkutano wa wake wa Marais wa Afrika na Mke wa Marekani, MIchelle Obama utakaofanyika kwenye kituo cha John F Kenedy

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni